Aliyekuwa Katibu mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Dr Peter Mathuki anatarajiwa kuhojiwa na Kamati ya sheria, Haki, na Hadhi ya Bunge la Jumuiya hiyo juu ya tuhuma zilizotolewa dhidi yake ikiwemo ya matumizi mabaya ya madaraka,ofisi na mali za Jumuiya.
Rais wa Kenya William Ruto ametangaza Ijumaa wiki hii kuwa siku kuu ya kitaifa kuomboleza vifo vya watu 238 waliofariki kutokana na mafuriko.
Kenya, Uganda, Rwanda, DRC na Sudan Kusini zimeamua kuweka nguvu ya pamoja kufanikisha ujenzi wa reli ya mwendo kasi SGR inayopita Afrika Mashariki.
Idadi ya vifo kutokana na mafuriko nchini Kenya imevuka 200 tangu mwezi Machi, wizara ya mambo ya ndani imesema Ijumaa, huku kimbunga kikielekea pwani ya Tanzania.
Maelfu ya wafanyakazi duniani wameshiriki katika sherehe mbali mbali za kuadhimisha siku ya wafanyakazi ya Mei Mosi, wakidai nyongeza za mishahara na nafasi bora za ajira kutokana na kupanda kwa bei za chakula na mafuta.
Mwaka huu Sherehe za Siku ya Kimataifa ya Wafanyakazi zina hisia ya dharura ya kujitolea upya kwa haki za kijamii, wakati tunapopitia kipindi kigumu, ikiwa ni pamoja na mabadiliko ya hali ya hewa na mabadiliko ya haraka katika sehemu za kazi kutokana na maendeleo ya teknolojia.
Wakati Tanzania ikiadhimisha siku ya Muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar, uliotimiza miaka 60 Ijumaa, Rais Samia Suluhu Hassan amewataka vijana nchini humo kuuenzi na kuulinda muungano.
Jeshi la Kenya lilifanya operesheni Alhamisi kuwaokoa wahanga wa mvua kubwa iliyosababisha vifo vya darzeni za watu kote Afrika Mashariki katika muda wa mwezi mmoja uliopita.
Baadhi ya asasi za kiraia zinazotetea haki za binadamu nchini Tanzania zimepinga kauli ya mkuu wa mkoa wa Singida Halima Dendegu ya kuwakamata na kuwachukulia hatua watoto wa kike wanaopata ujauzito wakiwa shule.
Benki ya Dunia ilisema Jumanne kuwa imesitisha ufadhili wa mradi wa utalii na uhifadhi nchini Tanzania kufuatia madai ya ukiukwaji wa haki za binadamu.
Kituo cha sheria na haki za binaadamu kiimeitaka serikali kuwasilisha mswaada wa sheria wa kufanya mabadiliko ya katiba kutokana na baadhi ya marekebisho katika sheria hizo kushindwa kufanyika kutokana na mapungufu yaliyopo kwenye katiba ya nchi hiyo.
Wananchi nchini Tanzania wamelalamikia tatizo la upatikanaji wa maji katika maeneo mbalimbali, hali inayopelekea kutumia maji yasiyo safi na salama na kuwalazimu kina mama kutembea umbali mrefu kupata huduma hiyo.
Pandisha zaidi