Rwanda siku ya Jumapili ilipuuzilia mbali madai ya Burundi kwamba iliwapa silaha kundi la waasi linaloshutumiwa kwa milipuko ya guruneti na kujeruhi watu kadhaa, na kuzidisha uhusiano mbaya kati ya majirani hao wa Afrika Mashariki.
Rais wa Kenya William Ruto ametangaza Ijumaa wiki hii kuwa siku kuu ya kitaifa kuomboleza vifo vya watu 238 waliofariki kutokana na mafuriko.
Mwaka huu Sherehe za Siku ya Kimataifa ya Wafanyakazi zina hisia ya dharura ya kujitolea upya kwa haki za kijamii, wakati tunapopitia kipindi kigumu, ikiwa ni pamoja na mabadiliko ya hali ya hewa na mabadiliko ya haraka katika sehemu za kazi kutokana na maendeleo ya teknolojia.
Mamlaka ya Ufaransa inasema msichana mwenye umri wa miaka 7 alikuwa miongoni mwa wahamiaji watano waliozama kwenye mfereji wa bahari kati ya Uingereza na Ufaransa, maarufu English Channel,
Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo ni vyena iwasilishe malalamiko katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki juu ya Rwanda kushindwa kuheshimu mipaka yake, balozi ya Ubelgiji nchini Congo amesema siku ya Ijumaa katika mkutano wa kutathimini kwa undani mgogoro wa Mashariki mwa Congo.
Mwanamke wa Rwanda, aliyeondolewa Marekani, miaka mitatu iliyopita amehukumiwa kifungo cha maisha gerezani kwa kuhusika katika mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 nchini humo, gazeti la The New Times limeripoti Jumamosi.
Rwanda inajiandaa kuadhimisha miaka 30 ya kipindi cha kutisha zaidi katika historia ya taifa hilo ya mauaji ya halaiki dhidi ya Watutsi walio wachache.
Serikali ya Haiti iliomba rasmi msaada wa usalama kutoka kwa nchi zote kote duniani, zaidi ya mwaka mmoja uliopita.
Uchumi wa Rwanda unatarajiwa kukua kwa asilimia 6.6 mwaka 2024, ikilinganishwa na mwaka huu ambapo umekuwa kwa asilimia 6.2, Waziri wa fedha na Gavana wa Benki kuu wameandika barua kwa Shirika la Kimataifa la Fedha Duniani- IMF.
Kampuni ya kutengeneza chanjo za Covid-19 ya BioNtech inalenga kuanza utengenezaji kwenye kiwanda chake cha chanjo cha mRNA chini Rwanda kufikia 2025, maafisa wake wamesema Jumatatu, ikiwa kampuni ya kwanza ya kigeni kutengeneza chanjo hizo barani Afrika.
Tume ya uchaguzi ya Rwanda imesema Jumanne kwamba uchaguzi wa Rais na bunge utafanyika Julai 15 mwaka ujao, wakati rais Paul Kagame akiwania kwa mhula wa nne.
Waziri Mkuu wa Uingereza alikuwa anahangaika siku ya Jumatatu kutafuta kura za kutosha kwa ajili ya sera yake uhamiaji ya kuwapeleka wanaoomba hifadhi nchini Rwanda baada ya wabunge wa chama chake kusema mpango wa sheria ya dharura hauna nguvu ya kutosha
Pandisha zaidi